The House of Favourite Newspapers

Katiba Mpya Hiyoo! Rais Samia Aagiza Msajili Kuitisha Kikao Maalumu

0

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalum cha Baraza la vyama hivyo pamoja na kuanza mchakato wa Katiba Mpya.

Rais Samia ametoa maagizo hayo jana tarehe 6 Mei 2023 Ikulu , Chamwino, Dodoma ambapo amemtaka Jaji Mutungi kuitisha kikao hicho kwa lengo la kufanya tathmini utekelezaji mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya Vyama vingi vya siasa nchini.
Mbali na Jaji Mutungi kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na:-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro, Watendaji wa Taasisi mbalimbali.

Katika kikao hicho Rais Samia, ametoa maelekezo ya namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa Wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja kupitia sheria ya uchaguzi na ile ya vyama vya siasa.

MBUNGE SHIGONGO APANDA Mbegu KWA WANAFUNZI CHUO CHA MUHAS, WAASWA KUTUMIA UBUNIFU KUJIKWAMUA…

Leave A Reply