The House of Favourite Newspapers

Katiba Mpya Korea Kaskazini Yampaisha Kim Jong Un

A third-generation hereditary leader, Kim rules North Korea with an iron fist and the change will mean little [KCNA via Reuters]

BUNGE la Korea ya Kaskazini limepitisha mabadiliko ya kikatiba ya kumwinua zaidi kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, kuwa mkuu wa nchi (head of state), wadhifa aliokuwa nao babu yake (Kim Il Sung) ambaye ndiye mwasisi wa taifa hilo la kikomunisti.

Hatua hiyo imefuatia Kim kupewa wadhifa huo na pia kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo katika katiba mpya iliyopitishwa mwezi Julai mwaka huu ambapo wachunguzi wanahisi imelenga katika matayarisho na kufikiwa mkataba wa amani na Marekani baadaye.

Awali, Kim alikuwa akijulikana kama “kiongozi mkuu” aliyekuwa pia mkuu wa majeshi.

Comments are closed.