Wakati sikuku ya Krismasi ikiwa imemalizika jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo amesherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya Misa fupi ya kuwakumbuka wapendwa wake waliotangalia mbele za haki akiwemo baba yake mzazi Marehemu, James Bukumbi na Bi. Asteria Kapela ambao wote wapo mbele za haki.
Akiendesha ibada fupi Paroko wa Kanisa Katoliki Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja amewataka wakazi wa Bupandwa na vitongoji vingine vilivyoungana katika misa hiyo kutenda matendo mema yenye kuumpendeza mungu katika kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Amesema kuwa mwanadamu anapaswa kufanya yale yote yanayompendeza Mungu,kuoneshaa upendo kwa ndugu jamaa na marafiki hata kama upo katika ngazi mbalimbali za kiserikali ama kidhehebu kuonesha umoja na mshikamano ili hata ukifa matendo yako yampendeze mungu.
Kwa upande wa familia, Bi Leah Bukumbi amewataka wakazi wa Bupandwa kushikamana kattika shida na raha, kuimarisha upenndo ili kutokusababisha mgawanyiko. Amesema kuwa familia ya Bukumbi inawapenda sana wakazi wa Bupandwa na itahakikisha inashiriki katika shughuli zote za kijamii na kifamilia ili kuendeleza umoja waliouacha wazazi wao ambao siku ya leo wanaukumbuka kwa kuwaombea.