The House of Favourite Newspapers

Kauli ya Ramos Baada ya Kutemwa Kikosi cha Taifa

0

Hatimaye Luis Enrique amepanga kikosi chake cha Timu ya Taifa ya Hispania kuelekea michuano ya Euro 2020 inayotarajiwa kuanza Juni 11, 2021 huku akimtema nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos.

“Baada ya msimu mrefu wa mapambano na ugumu nakiri kuwa nimepitia mengi magumu na hili la Euro linaingia.

“Nimepambana kama ilivyo siku zote kwa mwili na nafsi yangu ili nirejee kwenye ubora wangu kwa 100% kwa ajili ya klabu na timu yangu ya Taifa ila sio kila muda mambo huwa vile tunadhani.

“Imeniuma sikuweza kuisaidia Real Madrid na kuipambania timu yangu ya Taifa, lakini sina budi kupumzika ili kurejea vyema kwa ajili ya klabu na Taifa langu.

“Kutoka moyoni nawatakia kheri Wachezaji wenzangu wa timu ya Taifa, nami nitakuwa nyumbani kuishangilia timu kama Watu wengine, kila la kheri Hispania,” amesema Sergio Ramos, Nahodha wa Real Madrid na Mchezaji wa Hispania.

Leave A Reply