The House of Favourite Newspapers

Kaze Ataja Mikakati ya Usajili Yanga SC

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amefichua kuwa hafikirii kufanya usajili wa kukurupuka katika kipindi cha dirisha dogo wala kuingia kwenye presha ya mashabiki kwani amepanga kutafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa.

 

Kaze ametoa kauli hiyo kufuatia kesho Jumanne kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili msimu huu ambapo Yanga tayari imepanga kuwatoa baadhi ya wachezaji kwa mkopo ili waweze kusajili wachezaji wapya ambao wanaamini watakuwa na msaada.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema kuwa anajua wanakwenda kwenye kipindi cha usajili lakini hatokubali kufanya usajili wa presha kwani amepanga kuchukua wachezaji watakaokuwa na uwezo wa kumsaidia katika kikosi chake.

“Najua kwamba tunaelekea katika usajili wa dirisha dogo ambalo nitalitumia kufanya maboresho katika maeneo ambayo naamini kwa sasa hayapo sawa, ligi ngumu kutokana na ushindani uliopo lakini haiwezi kuzuia kuwa na timu imara.

 

“Siwezi kusajili kwa sababu presha ya kile ambacho watu wanakiona, nataka kuchukua wachezaji ambao naamini wana sifa za kuisaidia timu kwa sababu katika kipindi hiki inakuwa ngumu kupata mchezaji bora kwa kuwa wengi bado wanafungwa na mikataba katika timu zao na ikishindikana, nitamaliza na hawa ambao tupo nao,” alisema Kaze.

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply