The House of Favourite Newspapers

Stamina Apagawishwa na Global Radio, Atambulisha Ngoma

0

RAPA mkali kutoka Morogoro anayeunda kundi la Rostam, Stamina ameshangazwa na ukubwa wa kampuni ya Global, baada ya kuona kuwa inamiliki vitu vingi ikiwemo studio nzuri ya radio ya +255 Global Radio, baada ya kufanya ziara Makao Makuu ya ofizi hizo yaliyopo Sinza Mori, jijini Dar.

 

Stamina alitinga +255 Global Radio kufanya mahojiano na kipindi cha +255 Global Radio, ambapo alipata nafasi pia ya kutambulisha mkwaju wake mpya aliompa shavu mwanadada Maua Sama, uliopewa jina la Nalewa Leo.

 

Akipiga stori baada ya kuutambulishwa mkwaju huo uliotoka Desemba 10 na kugonga views zaidi  laki tatu Youtube ukishika nafasi ya sita kwenye trending Stamina alisema ameshangazwa kuona studio nzuri ya radio ya Global kwani hakutegemea kuona kitu kuzuri kama hicho.

“Aisee unajua hii ndiyo mara ya kwanza nakuja hapa ndani, noma sana bonge moja la eneo, nitakuwa nakuja hapa mara kwa mara kama ambavyo nimewaambia kuwa kuanzia mwezi ujao, kuna mawe yanakuja, ila kwa sasa Nalewa Leo mashabiki wanatakiwa kuifuata sana mtandaoni huko,” alisema Stamina.

 

Mbali na Nalewa Leo kufanya balaa mtaani ndani ya siku nne tangu itoke, Stamina alisema kuwa, mwaka ujao atafanya balaa kubwa na akiomba Global Radio na Global Publishers kwa ujumla wake kuendelea kumsapoti na akitoa shukrani pia kwa kuwa miongoni mwa wasanii ambao walipewa nguvu na Global Publishers wakati anatoka.

 

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitashindwa kuishukuru Global, kwani mmetusaidia sana wasanii nikiwemo mimi kufika mahali fulani, hivyo msituchoke muendelee kutuunga mkono siku zote kwani muziki wetu bila watu kama nyinyi ni ngumu kutoboa,” aliongeza Stamina.

Issa Liponda

 

Leave A Reply