The House of Favourite Newspapers

Kenya Kujenga Mradi wa Gari Zipitazo Juu ya Nyaya

 

Serikali ya Kenya imeingia mkataba wa dola $57.2 millioni ambazo ni Ksh5.8 billioni (sawa na TZS 128.7 bilioni) na Kampuni ya Doppelmayr Group ya Austria kwa ajili ya ujenzi wa magari yanayotembea kwenye nyaya (cable cars). Kampuni ya Doppelmayr inatarajiwa kuanza rasmi ujenzi wa mradi huo wa kiteknolojia Mwezi Mei mwaka huu na kukamilisha mwaka 2020.

 

Wadhamini wa mradi huo ambao ni Trapos Limited na Kenya Ferry Services (KFS) zilisaini mkataba huo wa mabilioni ya pesa tangu Desemba mwaka jana ambapo mchakato wa ujenzi wa mradi huo sasa upo njiani.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa KFS, Bakari Gowa alitoa taarifa juzi Alhamisi kuwa, kwa sasa wataalam wanamalizia upimaji na uwekaji alama wa maeneo ya barabara ambapo mradi huo utaweza kupita kwa urahisi.

 

Kwa mujibu wa mkataba huo, baada ya Trapos Ltd kumalizana na wawekezaji hao, mradi huo utasimamiwa na Likoni Cable Cars Express Ltd kwa muda wa miaka 25 kwa ajili ya kuboresha na kufanya marekebisho katika maeneo yatakayoonekana yana hitilafu ndani ya hicho kipindi.

 

Imeelezwa kuwa, katika mradi huo ambao ni wa kwanza Afrika Mashariki na Kati, njia moja itakuwa na magari 22 ya kupitia kwenye cable angani huku kila gari likibeba abiria 38, jumla ya wasafiri 11,000 wanatarajiwa kupewa huduma kwa saa moja katika njia zote hivyo kufanya jumla ya abiria 180,000 kwa siku moja.

 

 

Baada ya mradi huo kukamilika, abiria watalipa nauli ya Ksh 20 ($0.20) hadi Ksh 100 ($0.98) kutegemeana na umbali anaokwenda. Aidha, Gowa amesema mradi huo utakuwa na faida kubwa kwa wakenya kwani utapunguza msongamano wa magari na foleni zisizo za lazima.

 

LIVE: RC MAKONDA ATATUA KERO ZA WANANCHI DAR

Comments are closed.