The House of Favourite Newspapers

Kenyatta, Museveni, Samia Wakumbuka Magumu 2021

0

MARAIS wa nchi tatu za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za Tanzania, Kenya na Uganda wametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 na kuelezea magumu na mafanikio yaliyozikumba nchi zao kwa mwaka uliopita.

 

Rais Samia Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania katika salamu zake za mwaka mpya, alisema mwaka 2021 Tanzania iliendelea kukabiliana na janga la Covid-19 lililosababisha kuzorota kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kutoka ukuaji wa asilimia saba mwaka 2019/2020 hadi asilimia 4.8 mwaka 2020/2021.

 

Alisema hali hiyo ilitokana na athari za kufungwa kwa mipaka, kusitishwa safari za ndege za kimataifa na kusitishwa baadhi ya shughuli za uzalishaji na kiuchumi kulikofanywa na mataifa ambayo kati yao ni washirika wakubwa wa biashara na Tanzania.

 

“Pamoja na athari za Uviko -19 tulikuwa na ukuaji chanya wa uchumi, tukiwa ni miongoni mwa nchi 11 zilizokuwa kiuchumi kati ya nchi 54 za Afrika. Hii ilisababishwa na kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji kiuchumi badala ya hatua za kuwafungia kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine,” alisema Rais Samia.

 

Rais Kenyatta Katika salamu zake, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa EAC, alisema nchi yake itaungana na nchi nyingine wanachama wa EAC kuikaribisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika jumuiya hiyo.

 

“Nyongeza hii inayosubiriwa kwa hamu itaifanya EAC kuwa na nguvu na uwezo mkubwa wa kutimiza ndoto ya Afrika Mashariki,”  alisema Rais Kenyatta.

Kwa sasa nchi sita wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Sudan Kusini, Rwanda, Uganda na Burundi.

 

Katika mkutano wa 18 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa EAC uliofanyika Desemba 22, mwaka jana, marais hao waliidhinisha mchakato wa kuipa uanachama DRC na kuiagiza Sekretarieti ya jumuiya hiyo kukamilisha hatua zilizobaki ili nchi hiyo itangazwe rasmi mwanachama wa saba wa EAC.

 

Katika salamu hizo, marais hao; Kenyatta (Kenya), Samia Suluhu Hassan (Tanzania) na Yoweri Museveni (Uganda) walibainisha namna Covid-19 ilivyoyumbisha maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao na kusisitiza wananchi wao kujitokeza zaidi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo, huku wakiendelea kuchukua tahadhari nyingine kujikinga dhidi ya maambukizi.

 

Rais Kenyatta alisema nchini Kenya hadi Desemba 31, 2021, watu 39 walikuwa wamelazwa katika vituo mbalimbali vya uangalizi maalumu nchini kote wakiwa na Covid-19. Alisema kati ya watu hao, 19 wapo kwenye usaidizi wa uingizaji hewa na 20 wapo kwenye oksijeni ya ziada,” alisema.

 

Kuhusu amani, haki, siasa na uongozi, alisema Kenya itaendelea kushikilia mfumo wa haki ambao haurejeshi unaoadhibu tu. “Ni maombi yangu kwamba, mwaka 2022 uwe ambao mengi yatapatikana ndani ya mipaka yetu, mwaka ambao uongozi utatawala juu ya siasa, mwaka wa uamuzi wa ujasiri dhidi ya uamuzi wa kutaka umaarufu.

Leave A Reply