The House of Favourite Newspapers

Omondi Awavaa Mapromota Kenya

0

MSANII maarufu wa vichekesho nchini Kenya, Eric Omondi ameweka masharti magumu kwa mapromota na waandaaji wa matamasha ya muziki nchini humo watakapokuwa wakiandaa matamasha na hafla mbalimbali kuanzia mwaka huu 2022.

Omondi amesema wasanii wote watakaoalikwa kwa kutumbuiza matamasha lazima walipwe kiasi kisichopungua asilimia 75 ya kiwango cha pesa walichokubaliana kabla, na asilimia 25 iliyobaki siku ya tukio husika.

Aidha, Omondi ameorodhesha idadi ya wasanii wa daraja ‘A’ ambao kamwe hawapaswi kulipwa chini ya Ksh 600k ambayo ni sawa na tsh milioni 12 kwa kila onesho moja. huku pia akiweka kundi la wasanii wa daraja B ambao kwa mujibu wake wanapaswa kulipwa kuanzia Ksh 450,000.

“Wasanii wote wa daraja ‘B’ lazima walipwe si chini ya Ksh 450K yaani Ethic, Trio Mio n.k. matukio yote lazima yawe na headline na msanii wa Kenya iwe Beyoncé anatumbuiza au la! Usalama lazima utolewe kwa wasanii wote,” aliandika Omondi.

Leave A Reply