The House of Favourite Newspapers

Kerr: Kiiza hayupo ila Mbeya City watakaa tu

0

kerr

Dylan Kerr.

Hans Mloli, Dar es Salaam

WAKATI mashabiki wa Simba wakiwa na hofu ya kumkosa mshambuliaji wao hatari, Mganda, Hamis Kiiza kwenye mechi dhidi ya Mbeya City, kocha wa timu hiyo, Dylan Kerr, amejinadi kuwa watashinda mchezo huo hata bila ya Kiiza.

Kiiza ambaye amefunga mabao matano kati ya mabao saba ya Simba, ana asilimia kubwa ya kuukosa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho Uwanja wa Sokoine, Mbeya kutokana na majeraha ya nyama za paja.

“Ninao mastraika wengi hapa wanaoelewa kazi yao uwanjani, hivyo haina tatizo, suala la ushindi lipo palepale, lengo ni kuifunga Mbeya City na kuondoka na pointi tatu muhimu, hakuna kingine zaidi ya hapo,” alisema Kerr.

Kocha huyo amejinadi kuwa nia yake ni kupata ushindi na kama hilo litawezekana, maana yake atavunja mwiko wa Simba kusumbuliwa na Mbeya City uwanjani hapo kila wanapokutana.

Leave A Reply