The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe aliibua suala la Messi, apiga hodi TFF

0

POPE1

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameibua hoja kuhusiana na suala la kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ huku akisema Simba haijapokea barua ya hukumu yake kuwa ni huru kabla hajajiunga na Azam FC.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliamua Singano kuwa mchezaji huru na baada ya siku chache akatua Azam FC.
Hans Poppe amesema hadi jana hawakuwa wamepata barua ya hukumu hiyo kutoka TFF kuhusiana na uamuzi huo.

“Pamoja na hivyo, sisi tumewaandikia barua TFF kuwaambia tunataka kujua, kwamba Simba imeonekana tumefoji mkataba, vipi imekuwa kimya? Watupe barua na maelezo kivipi.

“Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema angefuatilia hadi mwisho na jibu angetupatia. Vipi hadi sasa kimya?

“Kama itaendelea kuwa kimya hivi, tunaweza kuchukua hatua nyingine za kisheria, halafu tutaonekana kama sisi ni wakorofi. Kama wao wapo kimya, sisi tutalipeleka polisi na mahakamani hilo suala. Tuwashitaki kwa mtu kufoji saini,” alisema Hans Poppe.

Wakati suala hilo likiendelea, kulikuwa na lawama za figisu kwamba Messi tayari alishafanya mazungumzo na Azam FC hata kabla ya kushinda kesi hiyo.

Leave A Reply