The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Akina Seth, Rugemalira na Makandege Waondoa Maombi Ya Pre-Bargain Kwa DPP

0
Harbinder Seth na James Rugemalira wakitoka chumba cha mahakama kusikiliza kesi inayowakabili.

UPANDE wa utetezi kupitia  Mshtakiwa aliyekuwa Mwanasheria wa kampuni ya  kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege, ameondoa rasmi maombi yake ya kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP.

hiyo imekuja baada ya siku 45 zilizotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya mshtakiwa huyo kuisha bila yeye kuonana wala kufanya majadiliano ( Pre Bargain) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania( DPP.)
Makandege kupitia wakili wale, Alex Balomi ameieleza Mahakama hiyo leo Mei 6, 2021, wakati kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili yeye na  wenzake wawili ambao ni Harbinder Seth na James Rugemalira, ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.
Mwakandege na Seth waliandika barua za kukiri mashtaka yao na kuomba kupunguziwa adhabu ili waimalize kesi yao.
Ikumbukwe Februari 25, 2021, mahakama hiyo iliamuru majadiliano ya kukiri mashtaka yaliyowasilishwa kwa DPP dhidi ya Seth na Makandege, yasikilizwe ndani ya siku 30, kuanzia siku hiyo.
Pia Aprili 8, 2021 mahakama hiyo iliongeza siku 15 ili washtakiwa hao kuendelea na majadiliano ya kukiri na mashtaka yao, lakini hadi sasa bado  hawajapata nafasi ya kufanya majadiliano dhidi ya DPP.
Wakili Balomi ametoa taarifa hiyo leo  baada ya wakili wa Serikali Faraji Ngukah kuieleza Mahakama hiyo, mbele ye Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, kuwa majadiliano ya kuimaliza kesi baina ya Seth na Makandege yanaendelea katika ofisi ya DPP.
” Mheshimiwa hakimu mazungumzo bado hayajafikiwa mwisho, bado yanaendelea hivyo tunaomba utuongezee muda kwa ajili ya kuendelea na mazungumzi baina ya washtakiwa na ofisi yetu” amedai Ngukah
Baada ya kueleza hayo,  mawakili upande wa utetezi likiongozwa na Michael Ngalo, John Chuma, Alex Balomi na Dorah Mallaba, kila mmoja aliwasilisha hoja juu ya upelelezi unavyochukua muda mrefu kukamilika,  majadiliano kutokamilika na kuiomba mahakama kuwafutia washtakiwa hao mashtaka na kuwaachia huru.
Wakili Dorah anayemuwakilisha mshtakiwa Seth amedai mteja wake bado hajakutana na wahusika kwa ajili ya kufanya majadiliano, hivyo kama majadiliano hayo yameshindikana waambiwe.
Kwa upande wake wakili wa Rugemalira, John Chuma ameendelea na ombi lake la kuitaka mahakama  iwafutie washtakiwa wote mashtaka yao na kuwaachia huru kwani ni miaka minne sasa imefika, kila siku wanaambiwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, akimtaka DPP atumie Mamlaka aliyonayo kutekeleza wajibu wake.
” Nilishasema tunapopewa nafasi kwenye hizi ofisi, tufanye kazi kama sheria inavyotutaka, tufanye kazi kwa haki na sio kutafuta maumivu , hivyo kila mmoja atimize wajibu wake ili kesi hii ifikie mwisho” amesema hakimu Shaidi.
Baada ya kueleza hayo, hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 20, mwaka huu itakapotajwa.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la kutakatisha fedha kiasi cha kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

 

Leave A Reply