The House of Favourite Newspapers

Mlipuko Beirut: Waziri Mkuu Lebanon Ajiuzulu

0

WAZIRI mkuu wa Lebanon, Hassan Diab, ametangaza kujiuzulu kufuatia mlipuko wa wiki iliyopita mjini Beirut. Kwenye taarifa yake fupi kupitia televisheni, Diab alisema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko.

 

Rais Michel Aoun amekubaliana na hatua hiyo ya serikali kujiuzulu. Wiki iliyopita Diab alimlaumu mtangulizi wake kwa mlipuko huo.

 

Alisema wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndiyo umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.

 

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuibuka baada ya mlipuko huo kutokea.

Leave A Reply