The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Kitilya, wenzake: Hakimu Awataka Wawe Wavumilivu

0

Hakimu Mkazi Kisutu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka akiyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Harry Kitilya na wenzake kuwa na wavumilivu wakati upelelezi wa kesi yao ya utakatishaji fedha inayowakabili kwa kuwa unakaribia kufika mwisho na mahakama ipo kwa ajili ya kutenda haki.

 

Kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, ambapo alisema watuhumiwa wawe wavumilivu kwani watapata haki yao ya msingi kwani upelelezi umekaribia hatua za mwisho.

Wakili wa Serikali Mwandamizi anayeendesha kesi hiyo, Kishenyi Mutalemwa, alieleza mahakama kuwa mara ya mwisho waliomba siku 14 ili waweze kuelezea hali ya upelelezi ulipofikia lakini wameshindwa, hivyo wakaomba kuongezewa muda ili tarehe ijayo waweze kuendelea na upelelezi huo na akaomba tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Baada ya Kishenyi kueleza hayo, wakili wa utetezi, Masumbuko Lamwai, alidai kuwa kesi ilifikishwa mahakamani hapo toka Aprili mwaka jana, hivyo mteja wake anazidi kuteseka gerezani bila kuleta ushahidi huo wa uchunguzi, hivyo akaomba wajitahidi kuharakisha upelelezi huo kwani watuhumiwa wanategemewa na familia zao.

 

Baada ya kutolewa kwa maelezo ya pande hizo zote mbili, Hakimu Mkeha amewaambia washtakiwa kuwa upelelezi unaofanywa unakaribia mwisho hivyo akawaomba wawe na imani juu ya upelelezi huo, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 5, mwaka huu

Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni maofisa wa benki ya Stanbic ambao ni Shose Sinare na Sioi Solomon.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa Dola milioni 6 za Marekani.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave A Reply