The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Pedeshee Ndama Yasogezwa Mbele Tena!

0

ndama-5

Ndama (katikati) na wenzake siku waliyopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza.

ndama-4

Kesi inayomkabili mfanyabiashara wa jijini Dar, Ndama Shaaban Hussein almaarufu Pedeshee Ndama Mutoto ya Ng’ombe, aliyewahi kuwa mfadhili wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ leo imesogezwa mbele hadi Januari 24, mwaka huu kwa madai kwamba upelelezi bado haujakamilika.

ndama-3

Pedeshee Ndama amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la utapeli wa dola za Kimarekani 540, 390 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1.18 ambapo anakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo kutengeneza nyaraka feki zikionesha kupata kibali cha kusafirisha sampuli ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

ndama-2

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa amemtaka mwendesha mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika mapema ili kesi hiyo ianze kusikilizwa na kutolewa hukumu.

ndama-1

Na Denis Mtima/ GPL

 

Leave A Reply