The House of Favourite Newspapers

KESI YA ZITTO MAUAJI YA UVINZA, UPELELEZI WAKAMILIKA – VIDEO

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imesema upelelezi wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe, umekamilika na sasa atasomewa maelezo ya awali ya kesi yake (Ph), Desemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Kesi hiyo namba 367 ya mwaka 2018 ya Zitto dhidi ya Jamhuri ya ambayo anashtakiwa kwa makosa matatu likiwemo la uchochezi na kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya polisi na raia wilayani Uvinza mkoani Kigoma, imeletwa kutajwa leo Jumatatu, Novemba 26 mahakamani hapo.

Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno,  katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema kuwa tuhuma alizotoa Zitto hazina ukweli wowote dhidi ya mauaji hayo na  hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

 

Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ” alisema Kamanda Ottieno.

BREAKING: ZITTO Afikishwa Mahakamani KISUTU/Mapya Yaibuka

Comments are closed.