The House of Favourite Newspapers

Khloe: Sina hisia zozote na Lamar Odom

0

Khloe-Kardashian-wearing-whiteKhloe Kardashian.

LOS ANGELES, Marekani
HII ina maana kuwa ndoto za Lamar Odom kurudiana na mkewe Khloe Kardashian, hazipo tena baada ya mrembo huyo kukiri hadharani kuwa hana hisia na staa huyo wa zamani wa NBA.

Khloe alionekana kutoa msaada mkubwa zaidi kwa Lamar alipopoteza fahamu akidaiwa kutumia madawa ya kulevya, hali iliyotafsiriwa kuwa huenda wangerudiana baada ya Lamar kupona.

151013-lamar-odom-khloe-kardashian_3ba208c377f91440912fae3dc080df5c.nbcnews-ux-2880-1000 (1)Mrembo huyo alisema kwa sasa Lamar atabaki kuwa rafiki na mfanyabiashara mwenzake huku ikidaiwa kuwa mrembo huyo anataka kuanza tena kufuatilia talaka yake mahakamani ili aachane naye jumla.

“Sidhani kama nina hisia na Lamar, nilikuwa karibu naye ili kumhudumia lakini watu wakatafuta sababu za kuongea. Nilitaka Lamar awe sawa na furaha pia. Kama ulikuwa pamoja na mtu kwa muda mrefu katika maisha lazima naye atakuwa nawe maishani,” alisema Khloe.

Chanzo kingine kilidai kuwa: “Lamar alitaka kumchumbia tena Khloe alisema wanataka wairudishe ndoa yao lakini Khloe alikataa akikumbuka namna alivyomsaliti na sasa anafuatilia talaka ili awe huru kutafuta mwanaume mwingine wa kumuoa.”

Leave A Reply