The House of Favourite Newspapers

ALI KIBA ALIVYOITEKA MWANZA NA SEDUCE ME

0
Alikiba akikamua.

MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ‘King Kiba’ usiku wa kuamkia jana aliliteka Jiji la Mwanza kupitia wimbo wake mpya unaofanya poa kwa sasa wa Seduce Me katika Tamasha la Tigo Fista 2017 lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.

 

Alikiba akifanya yake.

Katika tamasha hilo lililoanza saa 3:00 usiku kwa wasanii wachanga kupanda stejini kutoa burudani kwa upande wa magwiji wa Bongo Fleva walianza kupanda saa 5:30 usiku ambapo Rosa Ree alianza kuwakonga nyoyo mashabiki akifuatiwa na Lulu Diva kisha Rayvanny ambao walipokea shangwe za kutosha.

 

Wengine waliotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Fid Q, Ommy Dimpoz, Darassa, R.O.M.A, Nandy, Stamina, Aslay, Saida Karoli, Ben Pol na wasani wengine kibao.

Pamoja na wote hao kutangulia kutoa burudani, ilipofika zamu ya Alikiba majira ya saa 9:15 uwanja mzima ulizizima kwa burudani, shangwe zikawa za kutosha hasa alipotumbuiza wimbo wake mpya wa Seduce Me.

Makamuzi yakiendelea.

Mara baada ya Alikiba kushuka stejini baadhi ya mashabiki wa burudani walianza kuondoka kuashiria kuwa nyoyo na kiu yao ya kupata burudani wameridhika vilivyo licha ya wengine kuendelea kudai aendelee na shoo.

Tigo Fiesta 2017 yenye kauli mbiu ya ‘Tumekusoma’ itaendelea wikiendi ijayo katika Mkoa wa Kigoma na mwaka huu inatarajiwa kufanyika mikoa 15 ya Tanzania Bara.

Mobeto: Diamond Hana Mwanamke Anayempenda Zaidi Yangu!

Leave A Reply