The House of Favourite Newspapers

Kiba, Diamond Wamkacha Shehe Mkuu

shehe-1-002 STORI:RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY, WIKIENDA

DAR ES SALAAM: Ama kweli imeshangaza wengi! Kitendo cha nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ally Saleh Kiba  kushindwa kutokeza kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaani Maulidi iliyofanyika wilayani Temeke jijini hapa ambapo walialikwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumuahidi kuwa wangefika.

Katika Maulidi hiyo ambayo ilifanyika Mtaa wa Liganga wilayani hapo na mwenyeji wa shughuli hiyo kuwa Shehe Alhad, ilihudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir na wengineo.

shehe-mkuu-14Shehe Mkuu wa Dar, Alhad Mussa Salum akiwa na waandishi na wahariri wa Global Publishers.

KAULI YA SHEHE MKUU JUKWANI

Wakati Maulidi hiyo ikiendelea, Shehe Alhad aliutangazia umati uliojaa kuwa, katika hafla hiyo aliwaalika wasanii mbalimbali na kuwataka watu kuwachukulia wasanii hao kama wenzao. Akiendelea kuweka mambo sawa, alisema mpaka muda huo msanii ambaye alishafika ni Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na pia akaongeza kuwa, msanii wa nyimbo za kughani, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ alikuwa njiani kufika eneo la tukio ingawa mpaka wageni waalikwa wanaondoka, Mpoto alikuwa hajafika.

Baadhi ya watu walifurika kwenye eneo hilo na kujua kuwa, Diamond na Kiba wangekuwepo, walishangaa kuona muda unakwenda bila wapendwa hao kuonekana licha ya kusubiriwa kwa hamu kubwa.

diamond-platnumz

Diamond

KAMA WANGEFIKA

Baadhi yao walisema kuwa, kama Diamond na Kiba wangejitokeza kwenye Maulidi hiyo, wanaamini Shehe Alhad angewaunganisha na kuwashikanisha mikono ya wengine wakiwa hawezi hata kuongea.

kiba-na-dioamond-2

Uokoaji huo ulishuhudiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga ambao walishiriki bega kwa bega na waokoaji tangu lilipotokea janga hilo. Kufuatia kufanikiwa kwa zoezi hilo, mashuhuda walilipuka kwa shangwe na kuwapokea wachimbaji hao ambao kati yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa ni kama walikuwa kuzimu na kwamba walikuwa na hofu kwa muda wote wakiamini walikuwa wamesahaulika.

ali-kibaAli Kiba

Kabla ya kuokolewa, yalifanyika mawasiliano ya kuwatumia ujumbe kwa kutumia waya ili waseme wako wangapi na majina yao, ambapo walisema kuwa wako 15 na kwamba walikuwa na njaa na walihitaji maji, soda na sigara. Akizungumza na Wikienda juu ya chanzo cha tukio hilo, msemaji wa mgodi huo, Fracis Kiganga alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mazingira duni ambayo siyo salama kutokana na uduni wa vifaa wanavyotumia mgodini humo.

kiba-na-dioamond-1 Mbali na Mchina huyo, Meng Juping, wengine waliookolewa ni Ezekiel Bujiku (20), Yohana Shigangama (34) na Aniset Masanja (32). Wengine ni Dikson Moris (25), Mussa Cosmas (28), Raphael Nzubi (26), Amani Silvester (26), Sheku Butogwa (22), Hassan Idd (31), Augustino Robert (27), Mgalula Kayanda (23), Sabato Philimon (30) na mmoja ambaye jina halikutambulika haraka.

upendo hali ambayo ingeweza kumaliza bifu lao. “Jamani hawa jamaa zetu kina Diamond ndiyo kusema hawaji au wameshaondoka? Nasikia nao walialikwa. Unajua ni kutokuwa na uelewa tu, kama wangefika, lazima wangepatanishwa. Hii ni hafla ya kidini ndiyo maana watu wa kidini wapo hapa. “Hakuna mahalipa kumaliza bifu kama hapa kwenye shughuli ya kidini. Mfano, wangekuwa na Shehe Alhad akawashikisha mikono si wangemaliza mambo yao?” alihoji mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hassan.

img_2758

Balozi Seif Idd

KAULI YA BALOZI IDD

Alipopewa nafasi ya kuongea katika shughuli hiyo, Balozi Seif Iddi alisema misikiti endapo itatumika kwa mujibu wa maelekezo ya Mtume Muhammad itaendelea kuwa kimbilio la waumini wote wa dini hiyo.

Makamu huyo wa rais, alisema kuwa, tabia ya baadhi ya waumini wa dini hiyo kuifanya misikiti kuwa majukwaa ya kisiasa ndiyo sababu kubwa inayoibua mafarakano katika jamii, yakiwemo mambo ya kugombea uongozi misikitini. Balozi Idd aliongeza kuwa, waumini na wananchi wanapaswa kujitahidi kuitumia misikiti mbali ya kusali lakini pia inaweza kufanywa sehemu ya mipango ya maisha, sehemu ya kutoa tiba, sadaka na michezo inayokubalika kiimani.

AGUSIA MADAWA YA KULEVYA

Pia kiongozi huyo wa ngazi ya juu serikalini Zanzibar alisema jamii inaendelea kushuhudia matumizi yasiyo sahihi ya matumizi ya madawa ya kulevya, udhalilishaji wa watoto wadogo, wanawake na ujambazi. Pia akasema: “Kuporomoka kwa maadili hasa kwa vijana kwa kiasi kikubwa kunatokana na kukosa fursa za kujifunza kupitia misikiti ndani ya muongozo wa kiongozi wa dini ya Kiislamu, Mtume Muhammad.”

sheikh-abubakar-zuberi-bin-allyShehe Zubeir

MUFTI MKUU NAYE ATOA NENO

Naye Mufti wa Tanzania, Shehe Zubeir alisema inasikitisha kuona fursa kama hiyo ikiwa ni miongoni mwa nyingi zilizopo kwa ajili ya kutekelezwa na waumini  lakini wapo baadhi ya watu wanaopiga vita. Alisema maendeleo yoyote, ikiwemo ya ibada yanapatikana sehemu yenye ushirikiano na umoja.

Akasema mifarakano ni ugonjwa unaostahili kuepukwa na Waislamu kwa vile inasababisha mtafaruku katika jamii. ATOA TAHADHARI Mufti alitoa tahadhari akisema kwamba, waumini wa dini ya Kiislamu iwapo hawatakubali kubadilika, Uislamu utaendelea kubakia vijiweni tu.

KUHUSU ELIMU

Akigusia suala la elimu, Mufti alisema kwamba, Uislamu na elimu ni kitu kimoja kinachomuwezesha mtu kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

5....Bilal-akiendelea-kusoma-hotuba-yake..jpgDk. Bilal

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU

Akitoa salamu zake katika Maulidi hiyo, Dk. Bilal alisema mikusanyiko ya waumini ni darasa linalowasaidia wahusika kuwa na upeo zaidi wa ufahamu wa dini yao. Dk. Bilal aliupongeza uongozi wa Msikiti wa Majmuati Islamia chini ya Imamu Mkuu, Shehe Alhad ambaye pia ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi wa kuandaa mkusanyiko huo aliosema unaongeza upendo, mapenzi na kujuana miongoni mwa Waislamu.

WALIOALIKWA MAULIDI

Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyoandaliwa na uongozi wa msikiti huo, yalishirikisha pia waumini wa madhehebu tofauti wa Tanzania, Kenya na wawakilishi wa mabalozi na taasisi za kimataifa zilizopo nchini Tanzania.

WAGENI WAALIKWA WAONDOKA

Baada ya Shehe Alhad kuwasindikiza wageni waalikwa, Wikienda lilimuweka chemba na kuanza kumuhoji kuhusiana na kutofika kwa Diamond na Kiba ambao ilisemekana aliwaalika. “Aaah! Ni kweli Diamond na Kiba niliwaalika na wote waliniahidi kufika lakini nashangaa mpaka muda huu hawajatokea, sijui ni kwa nini lakini hilo siwezi kulizungumzia zaidi isipokuwa hata mimi nashangaa,” alisema Alhad na kuomba aachwe aendelee na majukumu yaliyombana, ikiwemo

kuagana na wageni wengine. Wikienda liliwapigia simu Diamond na Kiba ili kutaka kujua kilichowasibu mpaka kushindwa kutokea kwenye mwaliko huo.

DIAMOND: “Ni kweli nilialikwa, lakini nilipata dharura ya kifamilia, niko Afrika Kusini.”

Kiba simu yake haikuwa hewani.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.