The House of Favourite Newspapers

Kiba, Meneja Wake Kimenuka!

0

 

Kimenuka? Upepo unadaiwa si mzuri kati ya mfalme wa Bongo Fleva, Ali Salehe Kiba ‘King Kiba’ na meneja wake, Esi Mgimba, Gazeti la IJUMAA limekukusanyia habari kamili.

TAARIFA ZA AWALI

Awali, zilianza kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwanamuziki huyo alimfukuza kazi meneja wake huyo kitambo, ila mapema wiki hii ndipo taarifa zikaanza kuvuma kwa kasi kama moto wa kifuu.

 

“Ni muda kidogo tangu jamaa amteme meneja wake Esi, sema watu wengi walikuwa hawajui mpaka juzikati ilivyokuja kuvuja,” kilieleza chanzo makini kilicho ndani ya Lebo ya Kings Music iliyo chini ya King Kiba.

SABABU ZATAJWA

Chanzo hicho kilieleza kuwa, sababu iliyomfanya Kiba amuengue meneja wake huyo ni kupishana kwenye utendaji.“Kiba alishazoea kuachia wimbo mmoja mwaka mzima, yeye (meneja) akajifanya anataka mwanamuziki wake atoe nyimbo nyingi, ndicho kilichomponza,” kilieleza chanzo.Jambo hilo lilizua gumzo la aina yake mara baada ya kuvuja ishu hiyo ambapo kila mtu alikuwa na mtazamo wake juu ya suala hilo.

 

WENGINE WAMBEBA

ESIKuna baadhi ya mashabiki walisema, Kiba ametofautiana na meneja wake huyo kwa sababu ana kasi nzuri ya kikazi, lakini yeye anataka kwenda taratibu.“Kiba hataki kupelekeshwa, anataka mambo ya kimwinyi, yale sasa mtoto wa kike (meneja) anataka kuona matokeo ya haraka, si unajua muziki ulivyo na ushindani…” aliandika mdau mmoja mtandaoni.

WENGINE WAMBEBA KIBA

Wengine walisema kuwa, huwenda Kiba ametofautiana na meneja wake huyo kwa sababu ameshindwa kutimiza malengo aliyowekewa na uongozi wa Kiba.“Mimi nasikia dada ameshindwa bwana kwenda na malengo ya kumfanya Kiba awe namba moja Bongo, ndiyo maana akaachana naye,” aliandika mdau mwingine mtandaoni.

UKWELI NI UPI?

Gazeti la IJUMAA lilimtafuta meneja huyo wa Kiba ili kuweza kujua ukweli ni upi katika mengi yanayozungumzwa ambapo alipopatikana alisema hawezi kuzungumzia ishu hiyo.“Kama kuna mabadiliko yoyote, Kiba ndiye anayeweza kuyazungumza,” alisema Esi.

KIBA AFUNGUKA

Baada ya kumalizana na meneja huyo, Gazeti la IJUMAA liliamua kumtafuta Kiba mwenyewe kisha kumbana ili ategue utata uliopo ambapo baada ya kupatikana, alikiri kuacha kufanya kazi na meneja huyo na kuongeza kuwa kwa sasa wapo kibiashara zaidi.Mahojiano kati ya Gazeti la IJUMAA na Kiba yalikuwa hivi;

 

IJUMAA: Mambo Kiba, ishu zinakwendaje?

Kiba: Poa, habari yako (anataja jina la mwandishi).

 

IJUMAA: Salama, kuna taarifa zinasambaa mitandaoni kuwa umemfukuza meneja wako Esi na sasa hufanyi naye tena kazi, hii imekaaje?

 

Kiba: Kwanza watu wajue kwamba yule hajawahi kuwa meneja wangu, ila kuna baadhi ya mambo tu kwenye muziki wangu ndiyo alikuwa anashiriki, jambo lingine sijamfukuza sema kwa sasa ‘nadili’ naye katika kazi zingine za biashara, siyo muziki.

 

IJUMAA: Kwa maana hiyo hahusiki tena na mambo yako ya muziki?

Kiba: Ndiyo, hahusiki tena na muziki wangu, isipokuwa anahusika tu katika kazi za biashara zangu.

Kiba aliishia hapo na hakutaka kuulizwa maswali zaidi kwa kuwa alikuwa kwenye mishemishe zake za kikazi.

 

TUJIKUMBUSHE

Disemba 2019, zilisambaa tetesi kuwa Esi ndiye meneja mpya wa Kiba ambaye amempindua aliyekuwa meneja wa mwanamuziki huyo, Christine Mosha ‘Seven’ ambapo hata hivyo mwanadada huyo alikanusha kuchukua nafasi ya Seven na kuongeza kuwa yeye cheo chake ni Music Talent Manager and Business Consultant wa Kiba na siyo vinginevyo.

 

Kabla ya kufanya kazi na Esi, Kiba alifanya kazi kwa muda mrefu sana na Seven wakiwa na Kampuni ya Rockstar 4000 na sasa yupo chini ya meneja mwingine aitwaye Aidan Seif.Kwa sasa, Kiba anajinasibu zaidi na lebo yake ya Kings Music ambayo pia imesajili wasanii wanaochipukia kwenye gemu.

BALAA la AZANIA Kwenye VIWANJA vya SABASABA, WAREMBO WAFURIKA…!

Leave A Reply