The House of Favourite Newspapers

Kiba Noma… Awapa Wazungu Mil. 300 Amfunike Mondi

0

STAA wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ anataka kuthibitisha kwamba, kweli yeye ni mfalme (king), Risasi Jumamosi limedokezwa.

Ili kukamilisha ndoto yake hiyo na kumfunika kabisa mshindani wake kibiashara kwenye muziki huu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Kiba amewamwagia Wazungu zaidi ya shilingi milioni 300 za Kitanzania ili wamfanyie ‘mavituzi’ ya hatari.

 

STUDIO YA KIFAHARI AFRIKA

Risasi Jumamosi linafahamu kwamba, fedha hizo ni kwa ajili ya kujenga studio yake ya muziki ya audio na video itakayokuwa ya kifahari zaidi barani Afrika.

 

WAZUNGU KUTOKA UTURUKI

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Kiba anajenga studio hiyo akiwatumia wataalam ambao ni Wazungu kutoka nchini Uturuki barani Ulaya.

“Jamaa ameamua kuwaziba watu midomo kwa sababu kuna watu wanachonga sana.

 

“King Kiba anafungua bonge la studio kwa kutumia jina la lebo yake ya Kings Music Records ambayo yeye ni mkurugenzi wake.

“Kwa harakaharaka, ukiacha gharama za Wazungu wanaomtengenezea studio kwa maana ya kuseti vifaa ambavyo vimeshafika kutoka Uturuki, fedha nyingi imetumika kwenye kukamilisha jengo la kifahari ambapo ndipo patakuwa makao makuu ya studio. Ni hapahapa Tabata (Dar).

 

KIFUATACHO…

“Baada ya jengo kukamilika, sasa kifuatacho ni kuseti vyombo, tayari kwa uzinduzi hivi karibuni.

“Mzee unaambiwa zile studio za Wasafi Records (zinazomilikiwa na Diamond au Mondi) ni cha mtoto.

“Labda niwadokeze tu baadhi ya vitu au vifaa vya bei mbaya ambavyo vipo ndani yake.

“Kuna monitors original za audio kutoka kwenye maganda yake. Kuna vifaa vingine kama keyboards midi, sound cards za audio, mixer za hatari ambazo siyo zile za njia tatu au nne, hiyo ni mashine ya njia kama 30 hivi.

“Vingine ni vitu kama kompyuta,

DAW, audio interface, microphones, headphones, cables, stands, pop filter na maiki za kisasa kabisa.

“Pia vingine ni vitu kama rack mount, power conditioner, microphone preamp, headphone amp, monitor manager na vingine kibao.

 

KAMA ZA MASTAA MAREKANI

“Unaambiwa ni studio kama zile za mastaa wa Marekani za Gold Star Sound, Muscle Shoals Sound, Sunset Sound Recorders, Motown Studios,

Electric Lady Studios, Sun Studios, Capitol Studios au Chase Park.

MILIONI 300 NA USHEE

“Jumla ya gharama zote ndiyo kama hivyo ni zaidi ya shilingi milioni 300 za Kibongo,” kiliweka nukta chanzo hicho.

 

RISASI KWA KIBA

Gazeti hili limekutana na mtu ndani ya familia ya Kiba yenye maskani yake Tabata-Sanene jijini Dar.

Nje getini kwa Kiba, mtu huyo anaomba kutokutajwa jina lake baada ya kuwabaini waandishi wetu.

Hata hivyo, anajibu maswali ya waandishi wetu kwa mkato;

Risasi Jumamosi: Tumemkuta Kiba?

Mtu: Hapana, hayupo, kwanza ni nani amewaambia anakaa hapa?

Risasi Jumamosi: Sisi siyo wageni hapa, tumeshakuja mara nyingi tu.

 

Mtu: Basi kama mna shida sana mfuateni kwenye nyumba yake nyingine.

Risasi Jumamosi: Kwani ana nyumba nyingine maeneo haya?

Mtu: Ndiyo, kwanza siyo moja.

Risasi Jumamosi: Kwani Kiba ana nyumba ngapi?

Mtu: Kwa hapa Tabata ana nyumba tatu.

 

Risasi Jumamosi: Unaweza kutuelekeza nyumba nyingine ilipo?

Mtu: Hapana.

Risasi Jumamosi: Tuachane na hayo, tumeambiwa Kiba anafungua studio kubwa hapa nyumbani, je, ni kweli?

Mtu: Ni kweli, lakini siyo kwenye nyumba hii.

Hata hivyo, wakati Risasi Jumamosi likitaka maelezo zaidi, mtu huyo aligoma kuendelea na mazungumzo na kuwataka waandishi wetu kuondoka maeneo hayo kwani Kiba hakuwa nyumbani.

 

MENEJA AFUNGUKA

Gazeti hili lilimtafuta Kiba kwa njia ya simu ya mkononi, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, lilipomtafuta mmoja wa mameneja wa Kiba, Aidan Seif alikiri kuwepo kwa projekti hiyo.

“Ni kweli, studio ni ya Kings Music Records.

Risasi Jumamosi: Tunasikia anatumia Wazungu kutoka Uturuki kukamilisha taratibu kabla ya uzinduzi. Je, habari hizi ni za kweli?

Aidan: Ni kweli, inajengwa na Waturuki.

 

Risasi Jumamosi: Ina ukubwa wa kiasi gani?

Aidan: Itakuwa ni studio kubwa zaidi Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Risasi Jumamosi: Je, ni kweli inagharimu zaidi ya milioni 300?

Aidan: Sina hesabu kamili hapa, lakini inagharimu zaidi ya shilingi milioni 200 hadi 300 za Kitanzania.

 

Stori: WAANDISHI WETU, DAR

 

 

Leave A Reply