The House of Favourite Newspapers

KIBABE, YANGA WAICHAPA PRISON

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu amefanikiwa kuweka usawa wa mzani katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika 75.

 

Prisons walikuwa wa kwanza kuona lango la Yanga baada ya kufunga kwa penati dakika ya 45 bao lililofungwa na Jumanne Elfadhil.

 

Mabadiliko aliyoyafanya kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kumtoa Juma Abdul dakika ya 68 na kuingia Amiss Tambwe yamesaidia kwa kuwa mpira wa kwanza wa Tambwe umesababisha penati.

 

Tambwe anafanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 85 baada ya mabeki wa Prisons kufanya makosa ndani ya 18 hali iliyofanya kuweza kumpa nafasi Tambwe kuandika bao la pili na kufunga bao la tatu dakika ya 90.

Kadi Nyekundu ya NGASSA, YANGA VS TZ PRISONS Mwamuzi Alichofanya: UCHAMBUZI

Comments are closed.