The House of Favourite Newspapers

KIBONDE Alijua ATAKUFA Akaacha WOSIA, Baba, Mtoto Wasimulia – VIDEO

Global TV imefika nyumbani kwa Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Marehemu Ephraim Kibonde, maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar na kuzungumza na Baba mzazi na mtoto wa kwanza wa marehemu Kibonde….

Baba mzazi wa Kibonde amesema ni kama mwanae alikiona kifo chake kwani mara ya mwisho alizungumza nae akiwa hospitali muda mfupi kabla ya mauti kumkuta na akamsisitiza sana Baba yake kuwaangalia wajukuu zake yaani watoto wake watatu ambao amewaacha…

Aidha Mtoto wa kwanza wa Kibonde anayeitwa Ephraim naye ameongeza kuwa hatomsahau baba yake kwa jinsi ambavyo alikuwa mchapakazi na mara ya mwisho alipowasiliana nae alimwambia kuwa anajiandaa kurudi Dar…

Mwili wa Kibonde umewasili jijini Dar usiku wa jana ukitokea mkoani Mwanza ambapo ndipo mauti yalipomkutia na unatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi Machi 08, katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar…

Comments are closed.