The House of Favourite Newspapers

WAZIRI MKUU MSIBANI – “Hivi Kweli KIBONDE Amefariki?” – VIDEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewasili nyumbani kwa Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Ephraim Kibonde, maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar kwa ajili ya kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.

Waziri Mkuu amesema serikali inatambua mchango wa Kibonde kwa Taifa na kifo chake kimekuwa ni pigo kubwa kwani ni cha ghafla na kila aliyepata taarifa za kifo chake swali la kwanza kujiuliza lilikuwa ni Kweli Amefariki? kwani juzi tu yeye ndiye aliyekuwa mshereheshaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Mwili wa Kibonde umewasili jijini Dar usiku wa jana ukitokea mkoani Mwanza ambapo ndipo mauti yalipomkutia…

Mwili wa Kibonde unatarajia kuzikwa keshi Jumamosi Machi 08, katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar…

Comments are closed.