The House of Favourite Newspapers

Kichuya kuivaa Al Ahly kivingine

 

Shiza Kichuya

WAKATI Simba wakitarajiwa kucheza leo Jumamosi dhidi ya Al Ahly ya Misri, aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya ataivaa timu hiyo kivingine kabisa.

 

Kichuya ambaye siku chache baada ya Simba kutua Misri aliuzwa kwenda timu ya Ligi Daraja la Pili nchini humo ijulikanayo kwa jina la Pharco, Jumanne ya wiki ijayo anatarajiwa kuwa uwanjani akiwa na kikosi cha ENPPI kitakachocheza dhidi ya Al Ahly.

 

Pharco baada ya kumsajili Kichuya kwa mkataba wa miaka miwili, imempeleka kwa mkopo kwenye kikosi cha ENPPI kinachoshiriki Ligi Kuu ya Misri ambacho Jumanne ya wiki hii kitacheza dhidi ya Al Ahly ukiwa ni mchezo wa ligi kuu nchini humo.

 

Kutokana na kufanyika kwa usajili huo, Simba ilimuondoa Kichuya katika orodha ya wachezaji wake ambao leo Jumamosi watacheza dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo kwenye Mji wa Alexandria ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi.

 

ENPPI kwa sasa wanakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Misri wakiwa na pointi 21 baada ya mechi 21.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.