Kidoa: Sina Ndoto za Kuwa Mwanamuziki

MUUZA nyago anayefanya poa kwenye video mbalim­bali nchini ‘Kidoa’ amesema kuwa hana mpango wa kuingia kwenye muziki kama wafanyavyo video queens wengine kwa sababu hana kipaji cha kuimba.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Kidoa alieleza kuwa ingawa anapenda muziki lakini hana mpango wa kuingia kwenye fani hiyo kama wenzake kwani hajui kuimba na hajawahi kutamani kuwa mwanamuziki hivyo akilazimi­sha kuingia atachemka.

“Napenda niendelee kuwa video queen na siyo zaidi ya hilo, sina mpango wa kuwa mwanamuziki na siwezi kuta­mani fani hiyo acha nibaki huku na nina furaha na hiki nikifanyacho ndiyo maana un­aona nafanya vizuri kwenye video mbalimbali,” alisema Kidoa.

Na Ally Katalambula | RISAI JUMAMOSI

Stamina, Darassa Kulipeleka Jiji Dar Live Sikukuu ya Idd Mosi


Loading...

Toa comment