The House of Favourite Newspapers

Nazi, Machicha na Mzaituni Katika Kuboresha Ndoa

0

LEO kwenye safu yetu nitakueleza mwanamke jinsi ya kumsaidia mumeo kumuondoa mchoko kwa kumsinga na kumfanyia masaji.

 

UFANYEJE MUMEO AKIRUDI KUTOKA KAZINI?

Kwanza mpokee, mkaoge vizuri.

 

Baada ya hapo chukua machicha ya nazi, hapa naongelea nazi iliyochunjwa tui yakabaki machicha yake, changanya na karafuu ya unga na bizari ya manjano na maji ya rose.

 

Andaa mkeka umlaze mwenzio, msugue na mchanganyiko huo wa machicha ya nazi mpaka uhakikishe uchafu wote na nongo zote zimeisha.

Wewe atakufanyia vivyo hivyo kisha mnaoga, mnajikausha vizuri.

 

Baada ya hapo, chukua mafuta ya mzaituni au ya nazi, mpake mwili mzima. Unaanza kumsugua taratibu kwa upendo huku ukimwambia maneno matamu.

 

Kisha chukua unga wa karafuu, umnyunyizie taratibu sehemu za mgongo na kiuno huku ukiendelea kumsugua ili kuondosha maumivu ya mgongo na uchovu.

 

Akipitiwa na usingizi, muache alale kama dk 20 hivi kisha muamshe akaoge, ukimuogesha pia ni vizuri.

 

Kwa kumfanyia haya mumeo pia ni tiba tosha ya ndoa, wanawake na wanaume siku hizi hatuna muda wa mambo haya, anza leo kufanya hivyo.

Leave A Reply