The House of Favourite Newspapers

Kifo cha George Floyd: Maandamano Yatanda Marekani -Video

0

 

Maandamano makubwa yanayofanyika kote nchini Marekani baada ya mmarekani mweusi George Floyd kufa mikononi mwa polisi katika jimbo la Minnesota yameibua wasiwasi kuhusu afya ya jamii.

 

Hofu iliyopo ni kwamba makundi makubwa ya waandamanaji huenda yakasababisha ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Baadhi ya viongozi wametoa wito kwa watu kuzingatia utulivu katika maeneo ambapo waandamanaji wenye hasira walivunja maduka na kuharibu magari ya polisi katika siku za hivi karibuni, viongozi hao pia wamegawa barakoa na kuwatahadharisha waandamanaji kwamba wanahatarisha maisha yao.

Hapo jana, gavana wa jimbo la Minnesota Tim Walz alielezea kuwa waandamanaji wengi hawazingatii maagizo ya kukaa mbalimbali na wala hawavai barakoa tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa wiki.

Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo hatua za kulegeza karantini zimeanza kuchukuliwa katika miji mingi nchini Marekani.

Leave A Reply