testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Chaiweka Matatani Kazi ya Mkuu wa Polisi Japan

0
Mazishi ya Bw Shinzo Abe

MKUU wa jeshi la Polisi Itaru Nakamura, ambaye alisema atajiuzulu ili kuwajibika, ndiye afisa mkuu zaidi kujiuzulu kuhusiana na mauaji ya Bw Abe.

 

Tukio hili limekuja baada ya kifo cha aliyekua waziri mkuu wa zamani Bw Abe aliyekua na umri wa miaka 67 kuuliwa na Mtuhimiwa ambaye alikamatwa baada ya tukio lililotokea Julai 8 katika mji wa Nara.

Waziri mkuu mstaafu wa Japan Shinzo Abe

Waziri huyo alikufa masaa machache baada ya kushambuliwa kwa risasi eneo la shingoni. Jeraha hilo liliharibu mshipa wa ateri.

 

“Ili kuchunguza upya ulinzi na kutoruhusu tukio kama hili kutokea, tunahitaji kuwa na mfumo mpya,” Bw Nakamura alisema alipokuwa akitangaza nia yake ya kuacha kazi.

 

Katika ripoti iliyotolewa na jeshi hilo la Polisi lilionyesha udhaifu uliopelekea kuuawa kwa kiongozi huyo.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply