The House of Favourite Newspapers

Kigogo Aliyeomba Kukiri Kosa Akamzike Baba’ke, Mapya Yaibuka

0

UPANDE wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mwanasheria wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege umesema bado hawajafikia muafaka wa mazungumzo baina yao na mshtakiwa huyo.

 

Makandege anayekabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola za Marekani 980,000, ameomba kufanya majadiliano na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) ili kukiri kosa.

 

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kutoa mrejesho wa majadiliano ya mazungumzo ya awali, ambapo hawajafikia muafaka wa mazungumzo baina yao.

 

Oktoba 20, 2021 Makandege aliomba tena kufanya mazungumzo na DPP kufanya majadiliano ya kukiri makosa yanayomkabili ili kupata nafasi ya kwenda kushiriki msiba wa baba yake mzazi.

 

Komanya amedai kuwa baada ya kutafakari DPP ameridhia kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka hivyo, kurekebisha kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa jinai.

Leave A Reply