The House of Favourite Newspapers

Kigogo TRA Anayedaiwa Kumlawiti Mtoto Anyimwa Dhamana

MAHAKAMA Kuu Zanzibar Vuga, imemnyima dhamana mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hassan Abuutwalib maarufu Kiringo ambaye anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 13 huko Fuoni Uwandani Visiwani Zanzibar.

 

Kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2018 ya kosa la jinai iliyowasilishwa mahakamani hapo ilianza kusikilizwa juzi na hakimu wa mahakama hiyo, Valestine Andrew Katema ambapo alitupilia mbali ombi la kumpa dhamana Kiringo kutokana na kosa lenyewe sambamba na sababu za maombi hayo kukosa nguvu.

 

Amesema, amefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuhofia usalama wa mshtakiwa, kutokana na jamii kuchoshwa na vitendo hivyo vilivyokithiri ambapo huenda wananchi wanaweza kujichukulia sheria mkononi. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 13, mwaka huu.

Comments are closed.