The House of Favourite Newspapers

Kiiza: Mmempa Bossou? Kazi mnayo

0

HAMISI-KIIZA.jpgMshambuliaji wa timu ya Simba, Hamis Kiiza.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
STRAIKA wa Simba, Hamis Kiiza ndiye wa kwanza anayefurahia kutokuwepo kwa mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga, sasa kawaambia mashabiki wa Simba: “Msikae nyumbani njooni uwanjani.”
Tangu mwanzo Kiiza alinukuliwa na gazeti hili akiomba Yondani na Cannavaro wasiwepo katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara badala yake acheze Vincent Bossou na Mbuyu Twite katika beki ya kati ya Yanga.
Yondani hatacheza leo kwani anatumikia adhabu ya kadi nyekundu na Cannavaro bado hajawa fiti kwani ndiyo kwanza ametoka kuuguza jeraha la enka.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kiiza alisema dua zake zimetimia kwa kiwango kikubwa za Yondani na Cannavaro kutocheza leo na sasa ana uwezo mkubwa wa kufanya anachotaka katika lango la Yanga.
“Cannavaro na Yondani wananijua vizuri tu hivyo ni rahisi kunizuia lakini Bossou hanijui, pia siyo mzuri kwenye kukaba, hivyo hawezi kunizuia nikitaka kufunga, nimefurahi sana.
“Mashabiki wa Simba waje kwa wingi uwanjani kuona ninavyowafanya Yanga, hakika watafurahia kwa kitakachotokea,” alisema Kiiza aliyewahi kucheza Yanga.

Leave A Reply