The House of Favourite Newspapers

Kiiza: Yanga hii, lazima niifunge

0

HAMISI KIIZAHAMIS Kiiza wa Simba ana uchungu wa kuachwa bila sababu ya msingi na Yanga, sasa amesema atahakikisha anaifunga timu yake ya zamani atakapokutana nayo Jumamosi ijayo.

Kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Simba mwanzoni mwa msimu huu, Kiiza raia wa Uganda, ataichezea timu yake dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kiiza ameichezea Simba mechi mbili za ligi na kufunga mabao mawili huku akiiwezesha kufikisha pointi sita katika nafasi ya tatu ikizidiwa kwa mabao ya kufunga na Yanga iliyo kileleni.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kiiza alisema anaiheshimu Yanga lakini anaamini heshima hiyo inaweza kupungua kidogo kwa kuhakikisha anaifunga katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

Kiiza alisema anajua akiifunga Yanga atachukiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao bado wanamheshimu, isipokuwa hana jinsi kwani anachofanya sasa ni kuitumikia Simba kwa mapenzi yote.

“Tangu nimeondoka Yanga, beki yao ni ileile, sasa nawajua, hivyo nina nafasi kubwa ya kufunga kwani ujanja na udhaifu wao naujua na ninachotakiwa kufanya ni kuongeza ujanja kidogo niwafunge,” alisema Kiiza.

“Nitakuwa makini pia katika njia zangu za ushindi kwani hata mimi mabeki wao wananijua ipasavyo, kwa hiyo itakuwa mechi ya kutegeana fulani hivi.”

Mabeki anaowazungumzia Kiiza ni wale wa kati, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani ambao alicheza nao Yanga kwa misimu zaidi ya miwili kabla hajaondoka msimu uliopita.

Hata hivyo, kwa muda mrefu Cannavaro amekuwa akisema hawezi kupata tabu katika harakati za kumzuia Kiiza asipate bao katika lango lao.

“Kiiza amecheza Yanga muda mrefu tunamjua uzuri na ubovu wake, sasa mtu kama huyo anapojinadi kuwa atatufunga sisi tunakaa kimya isipokuwa tutakutana uwanjani ambapo tutaonyeshana kazi,” alisema Cannavaro.

JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778CHAMPIONI

Leave A Reply