The House of Favourite Newspapers

Kijana Auawa Bar Kisa Mwanamke

0

Jeshi la Polisi mkoa wa mwanza linawashikilia watu watano kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo mauaji.

 

Tukio la Kwanza
Huko maeneo ya Bar ya California, kata ya Ibisabageni, Wilaya ya Sengerema, Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji watu wawili kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Zacharia Mussa, miaka 26, Msukuma, mkulima, mnadani yaliyotokea tarehe 21.02.2021 majira ya 23:30 hrs.

 

Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni ugonvi uliotokana na wivu wa kimapenzi ambapo watuhumiwa hao walimjeruhi kwa kitu chenye ncha kali na baadae akapoteza maisha. Wanahojiwa kwa kina na mfumo wa kisheria utafuatwa ili kufikishwa mahakamani.

 

 

Tukio la Pili

Tarehe 22/02/2021 majira ya 03:00hrs huko maeneo ya Magela, kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana, watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kumjeruhi hamidu kamugisha, miaka 22, Mhaya, mkulima na mkazi wa Buhongwa.

 

Kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali ubavu wa kushoto. Chanzo cha tukio hili ni ugomvi uliotokana na pesa walizokua wakidaiana. Watuhumiwa wa kujeruhi ni:- Jackson Lucas, miaka 19, muha, mkulima wa Buhongwa. Na wenzake wawili.

 

 

Tukio la tatu

Tarehe 20/02/2021 majira ya 13:30hrs huko kituo cha mabasi buzuruga, wilaya ya nyamagana, askari polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bhangi yenye uzito wa kilogramu 200 ambayo ilitelekezwa na watuhumiwa baada ya kubaini wanafuatiliwa. Watu hao watakamatwa na watafikishwa mahakamani.

 

 

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea na msako mkali katika maeneo yote, majini na nchi kavu kwenye mitaa, kata na vijiji ili kuweza kubaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

 

 

Pia linatoa wito kwa wananchi pindi wanapokua na migogoro ya kifamilia wasijichukulie sheria mkononi bali wafuate taratibu za kisheria na washirikishe taasisi nyingine zikiwemo za dini kwa utatuzi mzuri wa migogoro hiyo.

 

 

Imetolewa na;

Muliro J. Muliro- ACP
Kamanda wa polisi (m) Mwanza.
24 Februari, 2021.

Leave A Reply