The House of Favourite Newspapers

Kizimbani kwa Kulima, Kusafirisha Bangi

0

RAIA wawili wa  Poland, Damien Jankowski na  Krzysztof pamoja na  watanzania watatu leo Februari 24 wamefikishwa  mahakama ya hakimu mkazi Moshi kwa kosa la kulima, kuuza na kusafirisha dawa za kulevya aina ya Bangi.

 

Katika kesi hiyo, Damien amesomewa mashtaka mawili likiwemo kulima na kusafirisha dawa za kulevya (Bangi) na nje ya nchi kinyume na sheria.

 

Damien licha ya siku ya tukio kukiri mbele ya vyombo vya habari,  kulima na kusafirisha bangi nje ya nchi, leo mbele ya mahakama amekana shitaka hilo na kusema hakuwai kulima bangi alikua analima maua.

Aidha mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo Eliwaza Pyuza, Mtanzania ambaye ni mke wa Mshtakiwa namba moja, Damien amesomewa mashtaka mawili likiwemo la kulima na kutumia dawa za kulevya aina ya bangi,na amekana mashtaka hayo huku akisema hajawai kujihusisha na dawa za kulevya kwenye maisha yake.

 

Naye mshtakiwa namba tatu katika kesi hiyo ambaye ni mtanzania Hanif Kanan amesomewa shitaka la matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

 

Aidha upande wa serikali kupitia kwa ofisi ya mkemia mkuu wa serikali umekwisha wasilisha ushahidi wake mbele ya mahakama kupitia vipimo na vielelezo vilivyochukuliwa siku ya tukio.

Leave A Reply