The House of Favourite Newspapers

Kijana Hamisi Afariki Dunia – Video

0


KIJANA Hamisi Salum (21) aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu amefariki dunia akiwa nyumbani kwao Tandika jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.

 

Hamisi alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu kwa muda mrefu, ambapo miaka kadhaa iliyopita Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na wadau wengine walimsafirisha kwenda nchini India kwa matibabu ambako alifanyiwa upasuaji kisha kupata nafuu na kuruhusiwa kurejea nchini.

 

Lakini mwanzoni mwa mwaka 2019 alizidiwa tena na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wasanii mbalimbali nchini wakijitoa kugharamia matibabu yake, ambapo alipatiwa matibabu kisha kupata nafuu na kuruhusiwa   kurejea  nyumbani huku akiendelea na matibabu madogo madogo mpaka umauti ulivyomkuta.

 

Tunamuombea Hamisi apate pumziko la milele.

 

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.

Leave A Reply