The House of Favourite Newspapers

 Kijana: Nusura P-Funk Aniue!

Pendael Timotheo akiwa chini baada ya kipigo.

 

“ILIKUWA nusura P-Funk, Majani aniue!” Hivyo ndivyo alivyoanza kusimulia kijana ambaye ni fundi wa kuchomea vyuma (welding), Pendael Timotheo, alipokuwa akilisimulia Ijumaa Wikienda namna alivyobondwa na mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva anayemiliki Studio ya Bongo Records, Paul Matthysse almaarufu P Funk au Majani.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilijiri usiku wa Jumatano ya wiki iliyopita kwenye duka (kontena) lililopo jirani na nyumbani kwa Majani, Bamaga- Mwenge jijini Dar.

 

P-Funk.

Mmoja wa mashuhuda hao walilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, Majani alikuwa akimlalamikia Pendael kumpigia makelele akiwa nyumbani kwake na kumuonya mara kwa mara kuwa aondoke mahali hapo, lakini hakufanya hivyo.

Ilielezwa kwamba, baada ya Majani kuona anakerwa, alitoka nje na kumfuata Pendael kisha kuanza kumshambulia kwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili.

“Jamaa alianza kumfanyizia palepale. Pendael alipotaka kujibu mapigo, Majani alichukua chupa na kumkata nayo mkononi.

Akiwa chini baada ya kipigo.

 

“Yaani kama siyo jamaa kuipanchi ile chupa, naona ilikuwa ikielekea usoni na hivi sasa tungekuwa tunaongea mengine,” alisema shuhuda huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Ilidaiwa kuwa, wakati akiendelea kumshambulia, walitokea wasamaria wema na kumdhibiti Majani kwa kuwaita Polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) ambao walifika na kumkamata prodyuza huyo.

Habari zilizopatikana kituoni hapo zilieleza kuwa, baada ya kudhibitiwa, maafande hao walimpelaka Majani kituoni hapo na kumfungulia kesi ya shambulio la kudhuru mwili yenye jalada namba KJN/ RB/500/2018- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.

Akigalagala.

Ilidaiwa kuwa, baada ya kutupwa lupango usiku huo, juhudi za kumnasua kwa dhamana zilifanyika ambapo alichomolewa kesho yake (Alhamisi) akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda huku akiwa hoi, akisikilizia maumivu, kijana huyo alidai kwamba, Majani alimshushia kipigo cha hatari na kumsababishia kushonwa nyuzi tisa mkononi huku akikiri kwamba, kama siyo msaada alioupata kwa wasamaria wema, basi angekata roho.

“Hapa nilipo nasikia maumivu ya kufa mtu, kusema kweli ilikuwa nusura Majani aniue,” alisema Pendael.

STORI: Richard Bukos na Issa Mnally, Dar, IJUMAA WIKIENDA

 

MASKINI KIJANA HUYU! CHUPUCHUPU AUAWE NA P-FUNK!

Comments are closed.