The House of Favourite Newspapers

Kikundi cha Sauti ya Jamii Chawatunuku Vyeti Wanawake Shujaa

0
Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana wa Feminia (TGNP) Alphonsina Ambrose akizungumza kwenye hafla hiyo.

Katika kuelekea siku ya wanawake ambayo inatarajia kufanyika kesho Machi 8 wanawake wa Kikundi cha Sauti ya Jamii Kilichopo Kipunguni Dar wamefanya hafla ya kuwapongeza wanawake waliofanya mambo makubwa ya kuigwa katika jamii.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ili9yofanyika Kipunguni jijini Dar, Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana Wafeminia (TGNP) Alphonsina Ambrosi amesema kuwa wanawake wana wajibu wa kulea watoto wao katika mazingira mazuri tokea mdogo ili asije kulaumu akiwa mkubwa.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo.

“Wanawake ndio wenye majukumu mazito katika kulea watoto huko majumbani hivyo basi kila mzazi ahakikishe anamlea mtoto katika mazingira mazuri ili baadaye akikuwa aje kuwa bora.

“Mtoto anatakiwa kusaidiwa kufundishwa kutambua kitu kizuri au kibaya mfano mtoto anaweza akaharibu kitu au akawa mchokozi hata akiwa anacheza na wenzie sasa badala ya mama kumuekeza kwamba mwanangu hiki unachokifanya siyo kizuri utakuta mama anamuacha alafu badae mtoto anatenda akiona kwamba hichi ni kitu cha kawaida na mama anasema huyu ndio kashazoea wakati kumbe angemrekebisha tangu akiwa mdogo ingesaidia kunjenga katika msingi mzuri.

“Msaidie mtoto kujitambua akiwa bado mdogo mfano kumzuia bado mapema kushikwa shikwa maumbile mtoto ajue sehemu ambazo hapaswi kuguswa hasa sehemu za siri hii itapelekea mtoto kutambua na itamsaidia siku hizi mambo yamebadilika kuna watu wengine utakuta manamgusa gusa katika sehemu za siri hadi mtoto anakuwa anaona ni kawaida kwa hiyo hata akija kuwa mkubwa mfano watoto wa kiume kuwa na mashoga hii inatokana na mazingira ambayo mtoto amelelewa kumbe tunaona kwamba endapo mzazi angekuwa anamzuia kushikwa shikwa sehemu za siri tangu akiwa mdogo angeona tu kwamba hiki kitu si sahihi na kwa sasa jukumu lawalinda watoto ni la jinsia zote za kike na kiume.

Mwenyekiti wa Wajane kwenye kikundi hicho, Mboni Gamuya (kushoto) akipokea cheti kutokana na ushujaa alioufanya.

“Kumsaidia mtoto anapotoka shule kufanya kazi alizopewa na walimu, utakuta wamama wengine wanakuwa bize na majukumu kiasi ambacho wanshindwa hata kujua maendeleo ya mtoto shuleni hata kama anafanya vibaya mzazi hajui,  kwa hiyo wamama wajitahidi hata kama una majukumu tafuta muda wa kuwa karibu na mtoto na kumsaidia kazi zake alizopewa na mwalimu wake, “amesema.

Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani, Kipunguni Daniel Malagashimba amesema kuwa watawake wanatakiwa kuheshimiwa na kuthaminiwa.

“Kila mwanamke ana haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa na kutambuliwa utu wake, kulindwa dhidi ya ubaguzi, udhalilishaji, dhuluma, unyanyasaji, ukatili wa kijinsia na mila potofu.

“Mwanamke ana haki ya kushiriki bila ubaguzi katika uchaguzi na ngazi zote za maamuzi, kupata fursa za ajira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa zinazofanana, pia ajira yake kulindwa wakati wa ujauzito na pale anapojifungua na kupata huduma bora za afya ikiwemo afya ya uzazi na pia ana haki ya kumiliki mali.

Wageni waalikwa wakisikiliza kiumakini.

“Mimi nikiwa mwenyekiti wa mtaa wangu katika ofisi yangu nimewaweka wanawake kwa kutambua mchango wao wana uwezo wa kutatua kero levo ya familia na wana uwezo wa kutatua migogoro huwa nakwenda mara moja tu wiki na kiukweli wanafanya vizuri na ninawafundisha namna ya kuwa viongozi na natajia mwenyekiti wa mtaa ajaye atakuwa mwanamke,” amesema.

“Sambamba na hayo pia kituo kilitoa vyeti kwa wanawake ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika jamii mmoja wa wanawake hao ni Mboni Gamuya au mama Samia yeye amekuwa akifanya kazi na wanawake wajane na baada ya kutambua juhudi zake wakampa uwenyekiti.

Waliotunukiwa vyeti wakiwa nyuma ya meza.

“Nilianza kupigania haki za wakinamama wajane ikiwemo kunyang’anywa mali pindi wafiwapo na waume zao nikawapambania kwa wanasheria mbalimbali na wakarudishiwa mali zao kwa hiyo wakanichagua kuwa mwenyekiti wao na tulianza na michango kidogokidogo kwa kuwa wengi wa wajane ni wazee na sasa tuna akaunti yetu benki ambayo mmoja wetu akipata tatizo tunachukua pesa na kutatua tatizo lake, alimaliza kusema.

Leave A Reply