The House of Favourite Newspapers

Messi Mchezaji Bora La Liga

0

BAADA ya kufunga mabao saba katika mechi tano, staa wa Barcelona, Lionel Messi ameibuka kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Februari ndani ya La Liga ikiwa ni tuzo ya kwanza kwake msimu huu.

 

Mwezi Februari kwa Messi ulikuwa wa mafanikio kwake kwani alifunga mabao saba tofauti na ilivyokuwa kwa mwezi Januari.

 

Hakuna mchezaji ambaye alifunga idadi hiyo ya mabao kwa mwezi Februari zaidi ya Alexander Isak ambaye alifunga mabao manne katika mwezi huo.

 

Hata hivyo, kwa msimu huu wa 2020/21, Messi anakuwa mchezaji wa pili wa Barcelona kutwaa tuzo hiyo, baada ya kinda Ansu Fati kutwaa tuzo hiyo, Septemba mwaka jana.

 

Messi katika mwezi huo, rekodi zake zilikuwa bora licha ya Barcelona kuonekana kusuasua lakini amekuwa na uwezo wa kupachika mabao.

 

Februari aliisaidia Barcelona kushinda mechi kati ya tano ambazo walicheza ndani ya ligi hiyo.

 

Ikumbukwe mwezi Desemba mwaka jana, Messi alifunga mabao manne na kwa sasa kasi yake inaonekana sio ya kubeza katika kusaka Tuzo ya Ufungaji Bora msimu huu.

Leave A Reply