The House of Favourite Newspapers

KILIMANJARO STARS KUGOMBANIA CHALENJI CUP KENYA

0
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao akizungumza na waandishi wa habari.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kinatarajia kwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji Cup itakayoanza Novemba 25 hadi Desemba 9 nchini Kenya.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema kuwa timu itashiriki michuano hiyo ambayo haikufanyika kwa miaka miwili mfululizo tangu mwaka 2015.

 

“Timu yetu ya Kilimanjaro Stars, itashiriki Chalenji Cup itakayofanyika Kenya, lakini tumechaguliwa kuandaa michuano ya Cecafa chini ya miaka 17 (under 17) mwakani na timu yetu ya taifa ya wanawake nayo itashiriki michuano ya Cecafa kuanzia Disemba 12 hadi 22 nchini Rwanda,”alisema Kidao.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply