The House of Favourite Newspapers

Kilo 88 za Madawa ya Kulevya Zakamatwa Dar

0

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata kilo 88.27 za dawa ya kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine.

 

Akizungumza leo (Alhamisi) Juni 17, jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Mamlaka hiyo, Gerald Kusaya alisema dawa hizo zimekamatwa katika eneo la Kimara- Juni 2, 2021, majira ya saba usiku yakiwa yamepakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Prado ambalo lilikuwa limetelekezwa barabarani.

 

Alisema dawa hizo zimekamatwa baada maofisa wa TRA kulitia shaka gari hilo na kuanza kulifuatilia ambapo baada ya dereva wa gari hilo kubaini kuwa anafuatiliwa aliamua kulitelekeza.

 

“Baada ya dereva wa gari hilo kubaini anafuatiliwa alitelekeza gari na kukimbia, baada ya upekuzi wa kisheria kufanyika ndani ya gari kulipatikana na mifuko mikubwa mitatu aina ya sandarusi (viroba).

 

“Ndani yake ikiwa na pakiti 12 za dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 12.25 pamoja na kontena za plastiki 73 ndani yake kukiwa na dawa aina ya Methaphetamine zenye uzito wa kilo 76.02,” alisema Kusaya.

 

Leave A Reply