The House of Favourite Newspapers

Kinana Akutana na Balozi wa Marekani, Uhusiano Kati ya Tanzania na Marekani Kuimarishwa

0
MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright leo Aprili 11, 2022 Lumumba Dar es salaam

MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright,  jijini Dar es Salaam ambapo wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi ya Marekani katika Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza muda mfupi baada ya balozi huyo kuondoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Aprili 11 2022, Kanali Mstaafu Kinana alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya kawaida katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchi hiyo.

Leave A Reply