The House of Favourite Newspapers

Kinana Uso Kwa Uso Na Mbowe Kwenye Msiba Wa Lowassa

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulurhaman Kinana amekutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowasa nyumbani kwake Osyesterbay Jijini Dar es Salaam

Jumanne Februari 13, 2024 mwili wa Hayati Lowasa unatarajiwa kuangwa na viongozi na wananchi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Jumatano Februari 14 mwili wa Hayati Lowasa utapelekwa katika Kanisa la KKKT Azania Front kwa ajili ya ibada takatifu na kuaga.

Alhamisi Februari 15 mwili wa Hayati Lowasa utasafirishwa hadi jijini Arusha ambapo viongozi na wananchi watapata fursa ya kuaga katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alifariki Jumamosi, Februari 10, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na tangazo la kifo chake lilitolewa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango.

WAZIRI MKUU AHUTUBIA NYUMBANI KWA LOWASSA ULIPO MSIBA – ATAJA RATIBA ya KUUAGA MWILI – HADI MAZIKO


 

Leave A Reply