The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa Bunge Marekani Apigwa Risasi

0
Steve Scalise

Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Congress nchini Marekani, Steve Scalise, amepigwa risasi na kujeruhiwa alipokuwa akihudhuria mazoezi ya mchezo wa baseball miongoni mwa wabunge.

Yamkini watu wengine wanne wamejeruhiwa, katika shambulio hilo linalodaiwa na mashuhuda kuwa ni kisa cha umiminaji wa risasi katika Jimbo la Virginia mapema leo Jumatano.

Seneta wa Republican, Rand Paul, anasema kuwa alisikia mlio wa risasi ya kwanza, kisha ikafuatiwa na milio ya risasi.

Walinda usalama walijibu mashambulio hayo.

 

Bwana Scalise ambaye ni mwanachama wa chama cha Republican, anasemekana alipigwa risasi kwenye makalio, huku ikisemekana kuwa afya yake haimo hatarini kwani amefikishwa hospitalini kwa matibabu pamoja na walinzi wake ambao pia walijeruhiwa na mshambuliaji.

Idara ya Polisi huko Virginia, inasema kuwa imemtia mbaroni mshambuliaji.

Rais Donald Trump amesema kuwa: “Tumetamaushwa mno na janga hilo.”

Katibu wa mawasiliano wa Ikulu ya White House , Sean Spicerameandika katika mtandao wa kijamii wa tweeter kuwa Rais Donald Trump anajulishwa kuhusiana na shambulio hilo.

Leave A Reply