The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mchungaji Msigwa Awatolea Uvivu Wabunge wa CCM Mikataba Mibovu ya Madini

0

DODOMA: Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amewashukia wabunge wa CCM kuhusu mikataba mibovu ya madini kwa madai kwamba wao ndiyo walioshiriki kupitisha mikataba mibovu ya madini, mingi ikiwa imeletwa kwa hati za dharura.

Msigwa aliendelea kusema kwamba sera mbovu za chama cha mapinduzi ndizo zilizoifikisha nchi hapa ilipo ambapo wabunge wa CCM, kwa sababu ya wingi wao bungeni, hupitisha sheria kiushabiki badala ya kuchanganua kwa kina.

Mbunge huyo machachari, alisema mikataba mibovu ya madini, imesababisha mara nyingi wabunge wa upinzani watoke au watolewe bungeni, akitolea mfano awamu iliyopita ambapo kila wabunge hao wa upinzani walipokuwa wakiomba miswada ya madini waipitie, walikuwa wakinyimwa na ghafla ikapelekwa miswada mitatu kwa mkupuo, tena kwa hati ya dharura, ikitakiwa kupitishwa yote.

Alisema anachokifanya Rais Magufuli, ni kizuri kwa sababu hakuna mtu anayependa tuibiwe lakini hatumii sera za chama kwa sababu bado zinakumbatia ufisadi wa madini na anaongoza kama aligombea kupitia mgombea binafsi. Mchungaji Peter Msigwa.

MSIKIE MSIGWA AKIFUNGUKA

Leave A Reply