The House of Favourite Newspapers

Kipa Taifa Stars Ataka Kakolanya Asepe Simba

0

KIPA wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Ivo Mapunda, amemshauri kipa wa Simba, Beno Kakolanya, kuondoka klabuni hapo na kutafuta changamoto mpya kwenye timu nyingine ili kukinusuru kiwango chake.

 

Kakolanya amekosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kuanzia alipojiunga nayo akitokea Yanga huku langoni akikaa Aishi Manula.

 

Akizungumzia ishu hiyo, Mapunda ambaye aliwahi kuwa kipa wa Simba na Yanga kwa vipindi tofauti amemshauri Kakolanya kutafuta changamoto nyingine nje ya Simba kwa kuwa uwezo wake unamruhusu kucheza timu nyingine na akarudisha makali yake ya zamani kuliko kung’ang’ania Simba ambapo hapati nafasi.

 

“Mimi ningemshauri Beno atafute changamoto mpya nje ya Simba kwa sababu unaona hata sasa ambapo tayari Simba ni mabingwa na mechi zilizobaki hawana presha ya matokeo lakini hapangwi ujue kuna tatizo hapo.

 

“Beno ni kipa mzuri na ana uwezo mkubwa wa kucheza timu nyingine kwa mafanikio kuliko kukomaa ndani ya Simba ambapo hana uhakika wa namba,” alisema Mapunda ambaye ametumika Taifa Stars kwa muda mrefu.

Stori: Hussein Msoleka, Dar es Salaam

Timiza malengo yako leo kwa kutuma dau lako 500-2000 kwenda namba ya kampuni 551551 kumbukumbu namba weka namba zako 5 za ushindi zikifuatiwa na neno SHINDA. Mfano 12345 SHINDA

#ChezaPesaShindaPesa #SioKawaida#chezaglobal

Leave A Reply