Kirusi Kipya Chawapata Watu 35 China Mashariki, Watafiti Wathibitisha Athari Zake

Watafiti wamesema kuwa kirusi hiki kinapatikana kwa kiumbe kama Panya

WANASAYANSI wanafuatilia kirusi kipya kilicho athiri watu wengi mashariki mwa China, Novel Langya henipavirus (LayV) kimepatikana kwa wagonjwa 35 katika majimbo ya Shandong na Henan, wanasayansi wanadhani kwamba kirusi hiko kimetoka kwa wanyama.

 

Hakuna ushahidi kuwa LayV inaweza kusambazwa kati ya watu na watu, watafiti wamegundua kirusi hicho kinapatikana kwa kiumbe kama panya ‘Shrews’.

Wataalamu wamesema kuwa watu wasiwe na hofu kwani kirusi hicho haklina hatari sana

Taarifa hii ilitolewa na watafiti wa nchini China, Singapore, Australia pamoja na New England journal of medicine

 

Mmoja wa watafiti Wang Linfa wa Duke-NUS Medical School huko Singapore amewaambia China’s State-Run Global Times kirusi hiko cha LayV hakina athari kubwa hivyo haina ulazima kwa watu kuwa na hofu.

Imeandikwa: Peter Nnally kwa msaada wa mitandao

4295
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment