The House of Favourite Newspapers

Kisa Brands Outlets Idris Aondoka Marekani

0

MCHEKESHAJI na Muigizaji, Idris Sultan amesema ilibidi arejee Bongo Fasta kutoka Nchini Marekani, kwa lengo la kufungua Duka jipya la nguo za wakubwa na watoto la Brands Outlet, lililopo katika jengo la Palm Village Mikocheni Dar.

Kwa wiki kadhaa jamaa huyo hakuwepo Bongo, alienda zake Marekani kwa ishu zake nyingine. Duka hilo linalomilikiwa na kampuni ya Nafri International.co.tz, yeye akiwa kama balozi wa brandi (Brand amabasador) linajiuhusisha na uuzaji wa nguo za aina na jinsia zote kwa bei nafuu kabisa, huku wakitoa ofa maalumu ya punguzo hadi asilimia 90.

Akizungumzia kilichomrudisha Bongo mapema, Idris alisema: “Nimerudi kwa sababu nilitaka kuwa sehemu ya uzinduzi wa ili duka ambalo limekuja kama msaada wa watanzania wa hali ya chini lakini wanapenda kupendeza wao na familia zao, kwahiyo duka hili la Brands Outlet litawashika mkono watu wote wenye mahitaji ya kupendeza kwa nguo nzuri lakini wakiwa na pesa ndogo.”

Leave A Reply