The House of Favourite Newspapers

Kisa Corona, Chadema Yasema: ‘Hatuingii Bungeni’

0

 

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Ester Bulaya, ametangaza kuwa wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekubaliana kuanzia leo Mei 1, 2020, hawatoingia bungeni kuhudhuria vikao na watabaki nyumbani Dodoma kama tahadhari ya maambukizi dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

 

“Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma.  Niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa.
“Tunalitaka Bunge lisitishe Bunge kwa siku 21 kuruhusu wabunge na watumishi wote wa bunge kwenda karantini, kupima wabunge wote na watumishi wa bunge na familia zao kubaini ni wangapi wana maambukizi ya corona ili hatua stahiki zichukuliwe,” amesema Bulaya. 

Leave A Reply