The House of Favourite Newspapers

Kisa DNA ya Watoto, Mke Achezea Kipigo Nusura Auawe

0

MWANAMKE mmoja nchini Nigeria amechakazwa vibaya na mwanamume anayedhaniwa kuwa ni mume wake baada ya kutokea hali yenye utata dhidi ya watoto wao.

 

Imedaiwa kuwa, mwanaume huyo tajiri na mfanyabiashara alikuwa na mpango wa kuhamisha familia yake kutoka Benin kwenda Canada ndipo ubalozi wa nchi hiyo ulipohitaji Vipimo vya DNA kwa watoto wake hao watatu kwa kuhofia kuwa huenda alikuwa akitaka kusafirisha watu wasiokuwa na uhusiano naye kinyume cha sheria (human trafficking).

 

Vipimo vilikuja na majibu kuwa bwana huyo siyo baba halali wa watoto wote watatu hivyo ufanyike
Utaratibu mwingine wa kupata Visa na taratibu zingine za kisheria ili aruhusiwe kuingia Canada.

 

Alirudi nyumbani kumhoji mke wake juu ya baba halali wa watoto hao na kwa nini amekuwa msaliti kwa kiwango cha hatari kiasi hicho lakini hakupata majibu ya kueleweka.

 

Hivyo jamaa huyo aliamua amuue kabisa lakini watu wakawahi kuokoa uhai wa mwadada huyo huku meno manne yakiwa yameng’olewa kwa ngumi nzito nzito alizosukumiwa. Taarifa rasmi kuhusu kukamatwa kwa mwanaume huyo bado hazijatolewa.

 

Leave A Reply